Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 126 Bible en Swahili de l’est
Prière pour la restauration d’Israël
1 Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto. 2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu. 3 Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi. 4 Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini. 5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. 6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.