Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
1 Chroniques 20 Bible en Swahili de l’est
Prise de Rabba
1 Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza. 2 Samuel 11.1 Deutéronome 3.11 Amos 1.14 Ezéchiel 21.20 1 Rois 20.26 2 Kisha Daudi akamtwalia mfalme wao taji toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana. 2 Samuel 8.11-8.12 2 Samuel 12.30-12.31 1 Chroniques 18.11 3 Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawakata-kata kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote. Josué 9.23 Juges 8.16-8.17 Exode 1.14 1 Chroniques 19.2-19.5 2 Samuel 12.31