Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 26.3
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu! 3 Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima! Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi! 4 Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako? 5 Hao waliokufa watetema Chini ya maji na hao wayakaao. 6 Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko. 7 Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu. 8 Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake. 9 Husitiri uso wa kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake. 10 Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana. 11 Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake. 12 Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake. 13 Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio. 14 Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?

Cette Bible est dans le domaine public.