Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 114.1
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.Psaumes 81.5 Exode 13.3 Genèse 42.23 Exode 20.2 Esaïe 11.16
2 Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.Lévitique 11.45 Exode 29.45-29.46 Exode 25.8 Deutéronome 27.9 Exode 6.7
3 Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma.Psaumes 77.16 Exode 14.21 Josué 3.13-3.16 Exode 15.8 Psaumes 104.7
4 Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo.Exode 19.18 Habakuk 3.6 Juges 5.4-5.5 Psaumes 18.7 Habakuk 3.8
5 Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma?Habakuk 3.8 Jérémie 47.6-47.7
6 Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo?Psaumes 29.6 Psaumes 114.4
7 Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.Esaïe 64.1-64.3 Psaumes 96.9 Job 9.6 Michée 6.1-6.2 Psaumes 77.18
8 Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.Deutéronome 8.15 Psaumes 107.35 Nombres 20.11 Psaumes 105.41 Exode 17.6

Cette Bible est dans le domaine public.