Les paroles mensongères
1 Bwana, uokoe, maana mcha Mungu amekoma, Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.
Esaïe 57.1 Esaïe 59.13-59.15 Jérémie 5.1 Esaïe 1.21-1.22 Esaïe 59.4
2 Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
Romains 16.18 Psaumes 41.6 Jérémie 9.8 Psaumes 10.7 Psaumes 5.9
3 Bwana ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;
Apocalypse 13.5 Daniel 7.8 Daniel 4.30-4.31 Proverbes 18.21 Psaumes 17.10
4 Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?
Jacques 3.5-3.6 Jérémie 2.31 Jérémie 18.18 Genèse 3.5 2 Thessaloniciens 2.4
5 Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema Bwana, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Proverbes 14.31 Esaïe 33.10 Psaumes 34.6 Psaumes 10.12 Job 5.21
6 Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Proverbes 30.5 Psaumes 18.30 Psaumes 19.8 2 Samuel 22.31 Psaumes 119.140
7 Wewe, Bwana, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele.Psaumes 37.28 1 Pierre 1.5 Jude 1.1 Deutéronome 33.3 Psaumes 10.18
8 Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.
Esther 3.6-3.15 Juges 9.18-9.57 Michée 6.16 Proverbes 29.12 Job 30.8