Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 137
Bible en Swahili de l’est


1 Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. Ezéchiel 1.1 Ezéchiel 1.3 Esdras 8.31 Genèse 2.10-2.14 Daniel 9.3
2 Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. Ezéchiel 26.13 Esaïe 24.8 Apocalypse 18.22 Psaumes 33.2 Psaumes 81.2
3 Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. 1 Chroniques 16.7 Jérémie 26.18 Luc 21.6 Psaumes 9.14 Jérémie 31.12-31.13
4 Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni? Amos 8.3 Osée 9.4 Esaïe 49.21 Lamentations 5.14-5.15 Esaïe 22.12
5 Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau. Psaumes 102.13-102.14 Esaïe 62.1 Psaumes 84.10 Néhémie 2.2-2.3 Daniel 6.10-6.11
6 Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu. Ezéchiel 3.26 Psaumes 22.15 Lamentations 4.4 Philippiens 1.20 Matthieu 6.33
7 Ee Bwana, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ya Yerusalemu. Waliosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini! Abdias 1.10-1.14 Ezéchiel 25.12-25.14 Jérémie 49.7-49.22 Lamentations 4.21-4.22 Abdias 1.18-1.21
8 Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi. Apocalypse 18.6 Esaïe 13.1-13.22 Esaïe 14.4-14.24 Apocalypse 18.20 Esaïe 44.28
9 Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba. Esaïe 13.16 Osée 13.16 2 Rois 8.12 Nahum 3.10 Osée 10.14

Cette Bible est dans le domaine public.