Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 149.5 Bible en Swahili de l’est
1 Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa. 2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao. 3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie. 4 Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.5 Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.6 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao. 7 Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za watu. 8 Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma. 9 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya.