Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 149
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa. Psaumes 89.5 Psaumes 33.3 Hébreux 2.12 Apocalypse 5.9 Psaumes 22.25
2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao. Zacharie 9.9 Psaumes 95.6 Job 35.10 Psaumes 47.6 Psaumes 135.3-135.4
3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie. Exode 15.20 Psaumes 81.2 Jérémie 31.13 Esdras 3.10 Psaumes 150.3-150.5
4 Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. Psaumes 132.16 Psaumes 35.27 Psaumes 147.11 Esaïe 62.4-62.5 Hébreux 12.10
5 Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao. Job 35.10 Psaumes 63.5-63.6 Psaumes 118.15 Psaumes 42.8 1 Pierre 1.8
6 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao. Hébreux 4.12 Apocalypse 1.16 Psaumes 66.17 Néhémie 9.5 Luc 2.14
7 Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za watu. 1 Samuel 15.2-15.3 Apocalypse 19.11-19.21 Juges 5.23 Psaumes 137.8-137.9 Zacharie 14.17-14.19
8 Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma. Josué 12.7 Job 36.8 Juges 1.6-1.7 Josué 10.23-10.24
9 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya. Psaumes 148.14 1 Corinthiens 6.2-6.3 Deutéronome 32.42-32.43 Apocalypse 3.21 Esaïe 14.22-14.23

Cette Bible est dans le domaine public.