Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 61.7 Bible en Swahili de l’est
1 Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. 2 Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. 3 Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. 4 Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako 5 Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako. 6 Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.7 Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.8 Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.