Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 61.8 Bible en Swahili de l’est
1 Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu. 2 Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. 3 Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate. 4 Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako 5 Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako. 6 Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi. 7 Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.8 Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.