Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 18.8
Bible en Swahili de l’est


1 Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe; Hushindana na kila shauri jema.Proverbes 2.1-2.6 Proverbes 20.3 Ephésiens 5.15-5.17 Jude 1.19 Proverbes 14.10
2 Mpumbavu hapendezwi na ufahamu; Ila moyo wake udhihirike tu.Proverbes 12.23 Proverbes 1.7 Proverbes 17.16 Proverbes 13.16 Nombres 24.15-24.16
3 Ajapo asiye haki, huja dharau pia; Na pamoja na aibu huja lawama.Proverbes 29.16 Proverbes 11.2 1 Pierre 4.14 Psaumes 123.3-123.4 Matthieu 27.39-27.44
4 Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi; Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.Proverbes 20.5 Proverbes 13.14 Proverbes 10.11 Jean 7.38-7.39 Colossiens 3.16
5 Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.Proverbes 28.21 Lévitique 19.15 Proverbes 24.23 Proverbes 17.15 Deutéronome 16.19
6 Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina, Na kinywa chake huita mapigo.Proverbes 22.24-22.25 Proverbes 29.9 Proverbes 12.16 Proverbes 27.3 Proverbes 14.16
7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.Proverbes 13.3 Proverbes 10.14 Proverbes 12.13 Psaumes 140.9 Psaumes 64.8
8 Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.Proverbes 16.28 Lévitique 19.16 Proverbes 12.18 Psaumes 52.2 Proverbes 26.20-26.22
9 Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu.Proverbes 28.24 Proverbes 10.4 Proverbes 23.20-23.21 Matthieu 25.26 Hébreux 6.12
10 Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.2 Samuel 22.3 Esaïe 26.4 Psaumes 144.2 Psaumes 91.2 Psaumes 18.2
11 Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.Proverbes 10.15 Ecclésiaste 7.12 Job 31.24-31.25 Psaumes 49.6-49.9 Psaumes 52.5-52.7
12 Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.Proverbes 15.33 Proverbes 11.2 Proverbes 16.18 Ezéchiel 28.2 Ezéchiel 28.9
13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.Jean 7.51 Deutéronome 13.14 Proverbes 20.25 2 Samuel 16.4 2 Samuel 19.24-19.30
14 Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake; Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?Proverbes 15.13 Proverbes 17.22 Jacques 1.2 2 Corinthiens 12.9-12.10 Psaumes 147.3
15 Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.Proverbes 15.14 Psaumes 119.97-119.104 Luc 10.39 Proverbes 9.9 Proverbes 1.5
16 Zawadi ya mtu humpatia nafasi; Humleta mbele ya watu wakuu.Genèse 32.20 1 Samuel 25.27 Proverbes 17.8 Genèse 43.11 Proverbes 19.6
17 Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; Lakini jirani yake huja na kumchunguza.Proverbes 18.13 2 Samuel 19.24-19.27 2 Samuel 16.1-16.3 Actes 24.12-24.13
18 Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.Proverbes 16.33 1 Chroniques 6.63 1 Samuel 10.21-10.27 Néhémie 11.1 1 Samuel 14.42
19 Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.Actes 15.39 Genèse 4.5-4.8 Proverbes 16.32 Genèse 27.41-27.45 Genèse 37.3-37.5
20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.Proverbes 12.13-12.14 Proverbes 13.2 Proverbes 25.11-25.12
21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.Ephésiens 4.29 Matthieu 12.35-12.37 Colossiens 4.6 Proverbes 10.19-10.21 Jacques 3.6-3.9
22 Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.Proverbes 19.14 Proverbes 12.4 Proverbes 31.10-31.31 Ecclésiaste 9.9 Proverbes 8.35
23 Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.Jacques 2.3 1 Samuel 25.17 Jacques 2.6 Genèse 42.7 Genèse 42.30
24 Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.Proverbes 17.17 Proverbes 27.9 Jean 15.13-15.15 1 Chroniques 12.38-12.40 Matthieu 26.49-26.50

Cette Bible est dans le domaine public.