Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Esaïe 50.4 Bible en Swahili de l’est
Reproches de l’Éternel à son peuple
1 Bwana asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo naliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu. Deutéronome 32.30 Jérémie 3.8 2 Rois 4.1 Néhémie 5.5 Matthieu 18.25 2 Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu. Esaïe 59.1 Josué 3.16 Nombres 11.23 Exode 14.21 Genèse 18.14 3 Mimi nazivika mbingu weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa kifuniko chao. Apocalypse 6.12 Psaumes 18.11-18.12 Exode 10.21 Matthieu 27.45