Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 50.7
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo naliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.Deutéronome 32.30 Jérémie 3.8 Néhémie 5.5 Matthieu 18.25 2 Rois 4.1
2 Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.Esaïe 59.1 Josué 3.16 Nombres 11.23 Nahum 1.4 Esaïe 66.4
3 Mimi nazivika mbingu weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa kifuniko chao.Apocalypse 6.12 Psaumes 18.11-18.12 Exode 10.21 Matthieu 27.45
4 Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.Luc 21.15 Jérémie 1.9 Matthieu 11.28 Jean 7.15-7.17 Psaumes 119.147
5 Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma.Hébreux 5.8 Jean 14.31 Philippiens 2.8 Jean 15.10 Matthieu 26.39
6 Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.Matthieu 26.67 Marc 15.19 Marc 14.65 Matthieu 27.30 Esaïe 53.5
7 Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya.Esaïe 42.1 Hébreux 13.6 Ezéchiel 3.8-3.9 Esaïe 49.8 Psaumes 89.21-89.27
8 Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na anikaribie basi.Esaïe 41.1 Apocalypse 12.10 Romains 8.32-8.34 Esaïe 43.26 Job 23.3-23.7
9 Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mkosa? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala.Job 13.28 Esaïe 41.10 Psaumes 102.26 Psaumes 39.11 Esaïe 51.6-51.8
10 Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la Bwana, na kumtegemea Mungu wake.Jean 12.46 Esaïe 9.2 Hébreux 5.9 Psaumes 25.12 Esaïe 26.3-26.4
11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.Esaïe 28.15-28.20 Jonas 2.8 Romains 1.21-1.22 Matthieu 15.6-15.8 Romains 10.3

Cette Bible est dans le domaine public.