Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 31.12
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa katika mwaka wa kumi na mmoja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likanijia, kusema,Ezéchiel 30.20 Jérémie 52.5-52.6 Ezéchiel 1.2
2 Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri, na jamii ya watu wake, Je! Umefanana na nani katika ukuu wako?Ezéchiel 29.19 Ezéchiel 31.18 Ezéchiel 30.10 Apocalypse 10.11 Jérémie 1.17
3 Tazama, Mwashuri alikuwa mwerezi katika Lebanoni, wenye matawi mazuri, na kifuniko chenye uvuli, na kimo kirefu; na kilele chake kilikuwa kati ya matawi mapana.Esaïe 10.33-10.34 Daniel 4.10 Ezéchiel 17.22 Ezéchiel 17.3-17.4 Juges 9.15
4 Maji yalimlisha, vilindi vilimsitawisha; mito yake ilipita pande zote za miche yake; naye akapeleka mifereji yake kwa miti yote ya kondeni.Ezéchiel 17.8 Ezéchiel 17.5 Apocalypse 17.1 Apocalypse 17.15 Jérémie 51.36
5 Basi kimo chake kilitukuzwa kuliko miti yote ya kondeni, na vitanzu vyake viliongezeka; matawi yake yakawa marefu, kwa sababu ya maji mengi, alipoyachipuza.Daniel 4.11 Ezéchiel 17.5 Psaumes 1.3 Esaïe 36.4 Esaïe 36.18-36.19
6 Ndege wote wa angani walifanya vioto vyao katika vitanzu vyake, na chini ya matawi yake wanyama wote wa kondeni walizaa watoto wao, na chini ya uvuli wake mataifa makuu yote walikaa.Ezéchiel 17.23 Daniel 4.12 Matthieu 13.32 Daniel 4.21
7 Basi hivyo alikuwa mzuri katika ukuu wake, katika urefu wa matawi yake; maana mizizi yake ilikuwa karibu na maji mengi. 8 Mierezi ya bustani ya Mungu haikuweza kumficha; misunobari haikuwa kama vitanzu vyake, na miamori haikuwa kama matawi yake, wala bustanini mwa Mungu hamkuwa na mti wo wote uliofanana naye kwa uzuri.Ezéchiel 28.13 Genèse 13.10 Psaumes 80.10 Esaïe 51.3 Ezéchiel 31.16
9 Nalimfanya kuwa mzuri kwa wingi wa matawi yake; hata miti yote ya Adeni, iliyokuwa ndani ya bustani ya Mungu, ilimwonea wivu.Esaïe 51.3 Genèse 13.10 Ezéchiel 28.13 Genèse 37.11 Ezéchiel 31.16
10 Basi Bwana MUNGU asema hivi; kwa kuwa umetukuzwa kimo chako, naye ameweka kilele chake kati ya mawingu, na moyo wake umeinuka kwa urefu wake;Ezéchiel 28.17 Daniel 5.20 2 Chroniques 32.25 Daniel 4.30 Matthieu 23.12
11 mimi nitamtia katika mikono yake aliye mkuu kati ya mataifa; naye atamtenda mambo; nimemfukuza kwa sababu ya uovu wake.Ezéchiel 32.11-32.12 Daniel 5.18-5.19 Deutéronome 18.12 Nahum 3.18 Ezéchiel 23.28
12 Na wageni, watu wa mataifa watishao, wamemkatilia mbali na kumwacha; juu ya milima na katika mabonde yote matawi yake yameanguka, na vitanzu vyake vimevunjika karibu na mifereji yote ya nchi; na watu wote wa dunia wameshuka, wakitoka katika uvuli wake na kumwacha.Ezéchiel 28.7 Ezéchiel 35.8 Nahum 3.17-3.18 Ezéchiel 30.11 Habakuk 1.6
13 Juu ya magofu yake ndege wote wa angani watakaa, na wanyama wote wa jangwani watakuwa juu ya matawi yake;Ezéchiel 32.4 Esaïe 18.6 Ezéchiel 29.5 Apocalypse 19.17-19.18
14 kusudi mti wo wote, ulio karibu na maji, usijitukuze kwa sababu ya kimo chake, wala usitie kilele chake kati ya mawingu, wala mashujaa wake wasisimame katika kimo chao kirefu, naam, wote wanywao maji; maana wote wametolewa wafe, waende pande za chini za nchi, kati ya wanadamu, pamoja nao washukao shimoni.Ezéchiel 26.20 Psaumes 82.7 Ezéchiel 32.18-32.32 2 Pierre 2.6 Deutéronome 21.21
15 Bwana MUNGU asema hivi, Katika siku ile alipotelemka mpaka kuzimu naliamuru matanga, nalikifunika kilindi kwa ajili yake, nikiizuia mito yake, nayo maji makuu yalizuiwa; naliamuru Lebanoni kumwombolezea, na miti yote ya kondeni ilizimia kwa ajili yake.Nahum 2.8-2.10 Apocalypse 18.18-18.19 Malachie 3.4 Apocalypse 18.9-18.11
16 Niliwatetemesha mataifa kwa mshindo wa kuanguka kwake, hapo nilipomtupa chini mpaka kuzimu, pamoja nao washukao shimoni; na miti yote ya Adeni, miti iliyo miteule na iliyo mizuri ya Lebanoni, yote inywayo maji, ilifarijika pande za chini za nchi.Esaïe 14.15 Esaïe 14.8 Ezéchiel 26.15 Ezéchiel 27.28 Habakuk 2.17
17 Hao nao walitelemka kuzimuni pamoja naye kwa watu waliouawa kwa upanga; naam, wale waliokuwa mkono wake, waliokaa chini ya uvuli wake kati ya mataifa.Psaumes 9.17 Ezéchiel 31.6 Ezéchiel 31.3 Marc 4.32 Néhémie 3.17-3.18
18 Umefanana na nani, hivi katika utukufu na ukuu, kati ya miti ya Adeni? Lakini utashushwa pamoja na miti ya Adeni, hata pande za chini za nchi; utalala kati ya hao wasiotahiriwa; pamoja na hao waliouawa kwa upanga. Huyu ndiye Farao, na jamii yote ya watu wake, asema Bwana MUNGU.Ezéchiel 32.19 Ezéchiel 32.21 Ezéchiel 28.10 Matthieu 13.19 Jérémie 9.25-9.26

Cette Bible est dans le domaine public.