1 Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.
Osée 6.1 Osée 12.6 Osée 13.9 2 Chroniques 30.6-30.9 Ezéchiel 28.14-28.16
2 Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe.Hébreux 13.15 Luc 18.13 Psaumes 69.30-69.31 Psaumes 51.2-51.10 Matthieu 7.11
3 Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.
Psaumes 10.14 Psaumes 68.5 Psaumes 33.17 Osée 14.8 Osée 5.13
4 Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha.
Jérémie 3.22 Esaïe 57.18 Sophonie 3.17 Esaïe 12.1 Ephésiens 2.4-2.9
5 Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni.
Esaïe 35.2 Matthieu 6.28 Deutéronome 32.2 Job 29.19 Esaïe 27.6
6 Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.
Psaumes 52.8 Ezéchiel 31.3-31.10 Jérémie 11.16 Genèse 27.27 Psaumes 80.9-80.11
7 Na wao wakaao chini ya uvuli wake watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni.
Psaumes 91.1 Osée 6.2 Cantique 2.3 Esaïe 61.11 Zacharie 8.12
8 Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.
Esaïe 41.19 Job 34.32 Ephésiens 5.9 Galates 5.22-5.23 Jean 1.47-1.48
9 Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Psaumes 107.43 Proverbes 10.29 Sophonie 3.5 Jérémie 9.12 Daniel 12.10