Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Zacharie 5.8
Bible en Swahili de l’est


1 Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la chuo lirukalo.Esaïe 8.1 Zacharie 5.2 Jérémie 36.20-36.24 Ezéchiel 2.9-2.10 Jérémie 36.1-36.6
2 Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la chuo lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi.Zacharie 4.2 Amos 7.8 Apocalypse 18.5 Sophonie 1.14 2 Pierre 2.3
3 Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama ilivyo upande wa pili.Exode 20.15 Esaïe 43.28 Esaïe 48.1 Esaïe 24.6 Lévitique 19.12
4 Nitaituma itokee, asema Bwana wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba yake yeye aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.Lévitique 14.34-14.45 Proverbes 3.33 Habakuk 2.9-2.11 Job 18.15 Malachie 3.5
5 Ndipo yule malaika aliyesema nami akatokea, akaniambia, Inua macho yako sasa, uone ni kitu gani kitokeacho.Zacharie 1.9 Zacharie 2.3 Zacharie 4.5 Zacharie 1.14 Zacharie 1.19
6 Nikasema, Ni kitu gani? Akasema, Kitu hiki ni efa itokeayo. Tena akasema, Huu ndio uovu wao katika nchi hii yote;Amos 8.5 Ezéchiel 44.10-44.11
7 na tazama, talanta ya risasi iliinuliwa; na tazama, mwanamke akaaye katikati ya hiyo efa.Ezéchiel 16.1-16.63 Esaïe 15.1 Apocalypse 17.1-17.18 Osée 1.1-1.3 Ezéchiel 23.1-23.49
8 Akasema, Huyu ni Uovu; akamtupa chini katikati ya ile efa; akalitupa lile jiwe la risasi juu ya mdomo wa ile efa.Lamentations 1.14 Psaumes 38.4 Zacharie 5.7 Genèse 15.16 1 Thessaloniciens 2.16
9 Ndipo nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa kati ya dunia na mbingu.Osée 8.1 Matthieu 24.28 Deutéronome 28.49 Lévitique 11.19 Daniel 9.26-9.27
10 Ndipo nikamwambia yule malaika aliyesema nami, Hawa wanaipeleka wapi efa hii? 11 Akaniambia, Wanakwenda kumjengea nyumba katika nchi ya Shinari; tena ikiisha kutengenezwa, atawekwa huko mahali pake mwenyewe.Genèse 11.2 Genèse 10.10 Daniel 1.2 Jérémie 29.28 Esaïe 11.11

Cette Bible est dans le domaine public.