5 Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe. Marc 12.19 Luc 20.28 Matthieu 22.24 Genèse 38.8-38.9 Ruth 1.12-1.13 6 Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli. Deutéronome 29.20 Genèse 28.8-28.10 Ruth 4.10-4.12 Psaumes 9.5 Psaumes 109.13 7 Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu. Ruth 4.5-4.6 Ruth 4.1-4.2 8 Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu, Ruth 4.6 9 ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi. Ruth 4.7-4.8 Nombres 12.14 Esaïe 50.6 Job 30.10 Jean 1.27 10 Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu. 11 Washindanapo waume wao kwa wao, akakaribia mke wa mmojawapo, ili kumwokoa mumewe katika mkono wa ampigaye, yule mke akatoa mkono wake, na kumkamata tupu yake; 1 Timothée 2.9 Romains 3.8 12 umkate ule mkono wake, lisiwe na huruma jicho lako. Deutéronome 19.13 Deutéronome 19.21 Deutéronome 7.2