Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 14.14
Bible en Swahili de l’est


1 Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba.Esdras 3.7 2 Chroniques 2.3 2 Samuel 5.11-5.16 1 Rois 5.18 2 Chroniques 2.8-2.12
2 Daudi akajua ya kwamba Bwana amemweka imara ili amiliki juu ya Israeli, kwa kuwa milki yake imeinuka kwa ajili ya watu wake Israeli.Nombres 24.7 2 Samuel 7.8 Esaïe 1.25-1.27 1 Rois 10.9 Psaumes 89.20-89.37
3 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.Deutéronome 17.17 1 Chroniques 3.1-3.4 Ecclésiaste 9.9 Proverbes 5.18-5.19 2 Samuel 5.13
4 Na haya ndiyo majina ya watoto aliozaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani;1 Chroniques 3.5-3.9 2 Samuel 12.1 1 Chroniques 22.9-22.12 2 Samuel 5.14 1 Chroniques 28.5-28.6
5 na Ibhari, na Elishua, na Elpeleti;1 Chroniques 3.6 2 Samuel 5.15
6 na Noga, na Nefegi, na Yafia; 7 na Elishama, na Eliada, na Elifeleti.2 Samuel 5.16 1 Chroniques 3.8
8 Na waliposikia hao Wafilisti ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao.2 Samuel 5.3 Apocalypse 11.15-11.18 2 Samuel 5.17-5.25 Psaumes 2.1-2.6 1 Chroniques 11.3
9 Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kuteka nyara katika bonde la Warefai.1 Chroniques 11.15 1 Chroniques 14.13 2 Samuel 5.18 2 Samuel 23.13 Esaïe 17.5
10 Daudi akamwuliza Mungu, kusema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye Bwana akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako.Proverbes 3.6 1 Rois 22.15-22.17 Juges 4.6-4.7 1 Chroniques 13.3 1 Chroniques 14.14
11 Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, Bwana amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.Esaïe 28.21 2 Samuel 5.20 Psaumes 144.1 Exode 14.28 Psaumes 18.13-18.15
12 Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto.Exode 32.20 Exode 12.12 Deutéronome 7.5 Deutéronome 7.25 1 Samuel 5.2-5.6
13 Lakini hao Wafilisti wakateka nyara tena mara ya pili bondeni.1 Chroniques 14.9 2 Samuel 5.22-5.25 1 Rois 20.22
14 Na Daudi akamwuliza Mungu tena; naye Mungu akamwambia, Hutapanda kuwafuata; uwageukie mbali, ukawajie huko kuielekea miforsadi.Psaumes 27.4 Jean 9.6-9.7 1 Chroniques 14.10 Josué 8.2-8.7
15 Kisha itakuwa utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miforsadi, ndipo utakapokwenda nje vitani; kwa maana ndipo Mungu ametoka mbele yako, awapige jeshi la Wafilisti.Lévitique 26.36 2 Rois 19.7 Juges 7.9 Michée 2.12-2.13 Philippiens 2.12-2.13
16 Daudi akafanya kama vile Mungu alivyomwamuru; wakawapiga jeshi la Wafilisti toka Geba mpaka Gezeri.Jean 2.5 Exode 39.42-39.43 Jean 13.17 2 Samuel 5.25 Jean 15.14
17 Sifa za Daudi zikafika nchi zote; naye Bwana akawaletea mataifa yote hofu yake.Deutéronome 2.25 Exode 15.14-15.16 2 Chroniques 26.8 Josué 6.27 Josué 2.9-2.11

Cette Bible est dans le domaine public.