Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 26.14
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!Job 6.25 Job 6.12 Job 16.4-16.5 Job 12.2 1 Rois 18.27
3 Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima! Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi!Job 17.10 Job 33.3 Job 6.13 Proverbes 8.6-8.9 Job 38.2
4 Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?1 Rois 22.23-22.24 1 Corinthiens 12.3 1 Jean 4.1-4.3 Job 32.18 Ecclésiaste 12.7
5 Hao waliokufa watetema Chini ya maji na hao wayakaao.Psaumes 88.10 Genèse 6.4 Ezéchiel 29.3-29.5 Psaumes 104.25-104.26 Job 41.1-41.34
6 Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko.Psaumes 139.8 Proverbes 15.11 Amos 9.2 Job 28.22 Hébreux 4.13
7 Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.Job 9.8 Esaïe 40.22 Psaumes 104.2-104.5 Genèse 1.1-1.2 Esaïe 40.26
8 Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake.Proverbes 30.4 Jérémie 10.13 Esaïe 5.6 Genèse 1.6-1.7 Job 38.37
9 Husitiri uso wa kiti chake cha enzi, Na kulitandaza wingu lake juu yake.Psaumes 97.2 Exode 34.3 Job 22.14 1 Timothée 6.16 Exode 20.21
10 Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.Proverbes 8.29 Job 38.8-38.11 Jérémie 5.22 Psaumes 33.7 Genèse 8.22
11 Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake.1 Samuel 2.8 2 Pierre 3.10 Hébreux 12.26-12.27 Apocalypse 20.11 Aggée 2.21
12 Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake.Jérémie 31.35 Esaïe 51.15 Psaumes 89.9-89.10 Esaïe 51.9 Job 9.13
13 Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.Esaïe 27.1 Psaumes 74.13-74.14 Psaumes 104.30 Genèse 1.2 Psaumes 33.6-33.7
14 Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong’ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuelewa nazo?Psaumes 145.3 1 Samuel 2.10 Job 4.12 Psaumes 29.3 Job 11.7-11.9

Cette Bible est dans le domaine public.