Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 20.5 Bible en Swahili de l’est
1 Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. 2 Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. 3 Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. 4 Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote.5 Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote.6 Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu. 7 Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. 8 Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama. 9 Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.