1 Ee Bwana, nitakuita Wewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Psaumes 83.1 Psaumes 18.2 Psaumes 143.7 Psaumes 88.4-88.6 Proverbes 1.12
2 Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo, Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.
Psaumes 141.2 Psaumes 5.7 Psaumes 138.2 1 Timothée 2.8 Psaumes 134.2
3 Usinikokote pamoja na wasio haki, Wala pamoja na watenda maovu. Wawaambiao jirani zao maneno ya amani, Lakini mioyoni mwao mna madhara.Psaumes 12.2 Psaumes 55.21 Psaumes 26.9 Michée 3.5 Psaumes 62.4
4 Uwape sawasawa na vitendo vyao, Na kwa kadiri ya ubaya wa kufanya kwao, Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao, Uwalipe stahili zao.
2 Timothée 4.14 Apocalypse 18.6 Psaumes 62.12 Psaumes 59.12-59.13 Psaumes 21.10
5 Maana hawazifahamu kazi za Bwana, Wala matendo ya mikono yake. Atawavunja wala hatawajenga;
Esaïe 5.12 Psaumes 10.5 Osée 14.9 Esaïe 45.12 Jérémie 10.12-10.13
6 Na ahimidiwe Bwana. Maana ameisikia sauti ya dua yangu;
Psaumes 66.19-66.20 Psaumes 116.1-116.2 Psaumes 31.21-31.22 Psaumes 69.33-69.34 Psaumes 107.19-107.22
7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
Esaïe 61.10 Psaumes 30.11-30.12 Psaumes 13.5 Psaumes 69.30 Psaumes 56.3-56.4
8 Bwana ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.
Psaumes 20.6 1 Samuel 16.13 Esaïe 61.1 Psaumes 140.7 Psaumes 2.2
9 Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge, uwachukue milele.
Esaïe 40.11 Deutéronome 9.29 Psaumes 78.71 1 Rois 8.51 Esdras 1.4