Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 46
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Psaumes 145.18 Psaumes 9.9 Psaumes 62.7-62.8 Psaumes 91.1-91.9 Proverbes 18.10
2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Psaumes 23.4 Hébreux 13.6 Luc 21.33 Psaumes 27.3 Matthieu 21.21
3 Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. Psaumes 93.3-93.4 Jérémie 5.22 Esaïe 17.12-17.13 Nahum 1.5 Apocalypse 16.20
4 Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu. Apocalypse 22.1-22.3 Psaumes 48.1 Esaïe 8.6-8.7 Psaumes 87.3 Psaumes 36.8-36.9
5 Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema. Ezéchiel 43.7 Esaïe 12.6 Deutéronome 23.14 Ezéchiel 43.9 Zacharie 2.5
6 Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki; Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka. Amos 9.5 Psaumes 18.13 Nahum 1.5 Josué 2.24 Josué 2.9
7 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. 2 Chroniques 13.12 Psaumes 9.9 Nombres 14.9 Matthieu 28.20 Romains 8.31
8 Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. Psaumes 66.5 Psaumes 92.4-92.6 Exode 12.30 2 Chroniques 20.23-20.24 Esaïe 34.2-34.17
9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari. Esaïe 2.4 1 Samuel 2.4 Esaïe 60.18 Michée 5.10 Ezéchiel 39.3
10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi. Psaumes 100.3 Habakuk 2.20 Zacharie 2.13 Psaumes 83.18 Esaïe 2.17
11 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. Psaumes 46.7 Jérémie 16.19 Psaumes 46.1 Deutéronome 33.27 Psaumes 48.3

Cette Bible est dans le domaine public.