Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 52
Bible en Swahili de l’est


1 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote. Psaumes 94.4 1 Samuel 21.7 Psaumes 107.1 Psaumes 103.17 Psaumes 7.14
2 Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila Psaumes 57.4 Proverbes 18.21 Proverbes 12.18 Psaumes 59.7 Actes 24.5
3 Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. Psaumes 62.4 2 Timothée 3.4 Romains 1.25 Jérémie 9.8 Jérémie 9.3-9.5
4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila. Psaumes 120.3 Jacques 3.6-3.9 1 Samuel 22.18-22.19
5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung’oa katika nchi ya walio hai. Psaumes 27.13 Proverbes 2.22 Luc 16.27-16.28 Job 20.6-20.7 Apocalypse 21.8
6 Nao wenye haki wataona; Wataingiwa na hofu na kumcheka; Psaumes 40.3 Psaumes 37.34 Job 22.19 Psaumes 58.10-58.11 Apocalypse 18.20
7 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake. Job 31.24-31.25 Esaïe 14.16-14.17 Psaumes 49.6-49.20 Osée 12.7-12.8 Jean 19.5
8 Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele. Jérémie 11.16 Psaumes 13.5 Psaumes 92.12-92.14 Psaumes 1.3 Osée 14.6-14.8
9 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako. Psaumes 54.6 Psaumes 48.9-48.10 Psaumes 146.2 Psaumes 62.1 Psaumes 62.5

Cette Bible est dans le domaine public.