Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 98
Bible en Swahili de l’est


1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. Exode 15.6 Esaïe 52.10 Psaumes 96.1 Psaumes 96.3 Psaumes 33.3
2 Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Esaïe 52.10 Esaïe 62.2 Esaïe 49.6 Matthieu 28.19 Tite 2.13
3 Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Psaumes 22.27 Luc 1.72 Deutéronome 4.31 Psaumes 67.7 Actes 13.47
4 Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. Esaïe 44.23 Psaumes 66.1 Apocalypse 19.6 Psaumes 100.1 Psaumes 47.1-47.5
5 Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. Esaïe 51.3 Psaumes 92.3-92.4 1 Chroniques 25.1-25.6 1 Chroniques 15.16 Psaumes 33.2
6 Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana. Nombres 10.1-10.10 Psaumes 47.5-47.7 Apocalypse 19.16 2 Chroniques 29.27 2 Chroniques 15.14
7 Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. Psaumes 24.1 Psaumes 96.11-97.1 Esaïe 49.13 Esaïe 61.11
8 Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. Esaïe 55.12 Psaumes 65.12-65.13 Psaumes 47.1 Psaumes 89.12 Psaumes 93.3
9 Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili. Psaumes 96.13 Psaumes 96.10 Actes 17.31 Esaïe 5.16 Apocalypse 1.7

Cette Bible est dans le domaine public.