Dieu, le Roi juste et saint
1 Bwana ametamalaki, mataifa wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.
Psaumes 80.1 Psaumes 97.1 Exode 25.22 Psaumes 93.1 Esaïe 24.19-24.20
2 Bwana katika Sayuni ni mkuu, Naye ametukuka juu ya mataifa yote.
Psaumes 97.9 Psaumes 113.4 Esaïe 12.6 Jacques 4.6-4.7 Psaumes 66.7
3 Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa; Ndiye mtakatifu.
Josué 24.19 Deutéronome 28.58 Esaïe 6.3 1 Samuel 2.2 Psaumes 111.9
4 Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu; Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili; Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.
Psaumes 11.7 Jérémie 23.5 Esaïe 11.3-11.5 Apocalypse 19.16 Deutéronome 10.18
5 Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni penye kiti cha miguu yake; Ndiye mtakatifu.
Psaumes 132.7 Exode 15.2 Psaumes 34.3 Esaïe 25.1 Psaumes 99.3
6 Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia;Jérémie 15.1 Exode 24.6-24.8 Exode 14.15 Exode 15.25 Lévitique 8.1-8.30
7 Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao. Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa.
Exode 33.9 Nombres 12.5 Exode 40.16 Deutéronome 33.9 Hébreux 3.2
8 Ee Bwana, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
Nombres 20.12 Jérémie 46.28 Psaumes 89.33 Nombres 20.24 Nombres 14.20-14.34
9 Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Apocalypse 4.8 Psaumes 87.1-87.3 Luc 1.49 Habakuk 1.12 Esaïe 5.16