Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 99
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana ametamalaki, mataifa wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika. Exode 25.22 Psaumes 80.1 Psaumes 97.1 Esaïe 24.19-24.20 Psaumes 93.1
2 Bwana katika Sayuni ni mkuu, Naye ametukuka juu ya mataifa yote. Psaumes 97.9 Esaïe 12.6 Psaumes 113.4 Apocalypse 14.1-14.5 Hébreux 12.22-12.24
3 Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa; Ndiye mtakatifu. Esaïe 6.3 Josué 24.19 Deutéronome 28.58 1 Samuel 2.2 Psaumes 111.9
4 Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu; Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili; Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo. Psaumes 11.7 Jérémie 23.5 2 Samuel 23.3-23.4 Psaumes 98.9 Apocalypse 19.11
5 Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni penye kiti cha miguu yake; Ndiye mtakatifu. Psaumes 132.7 Psaumes 99.3 Exode 15.2 Psaumes 34.3 Esaïe 25.1
6 Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia; Jérémie 15.1 Exode 24.6-24.8 Exode 14.15 Exode 15.25 Exode 33.12-33.15
7 Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao. Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa. Exode 33.9 Nombres 12.5 Exode 19.9 Proverbes 28.9 Exode 40.16
8 Ee Bwana, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao. Nombres 20.12 Jérémie 46.28 Psaumes 89.33 Nombres 20.24 Nombres 14.20-14.34
9 Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu. Apocalypse 4.8 Psaumes 2.6 Psaumes 48.1-48.2 1 Samuel 2.2 Esaïe 6.3

Cette Bible est dans le domaine public.