Mission d’Ézéchiel
1 Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe.
Daniel 10.11 Ezéchiel 4.1 Ezéchiel 5.1 Actes 9.6 Ezéchiel 3.1
2 Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami.
Ezéchiel 3.24 Daniel 8.18 1 Samuel 16.13 Nombres 11.25-11.26 Juges 13.25
3 Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo.
Jérémie 3.25 1 Samuel 8.7-8.8 2 Chroniques 36.15-36.16 Jean 20.21-20.22 Romains 10.15
4 Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi.
Ezéchiel 3.7 Psaumes 95.8 Esaïe 48.4 Jérémie 6.15 Jérémie 5.3
5 Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao.Ezéchiel 33.33 Ezéchiel 3.27 Ezéchiel 2.7 Matthieu 10.12-10.15 Jean 15.22
6 Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma i pamoja nawe, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.
Jérémie 1.17 Jérémie 1.8 Michée 7.4 Esaïe 9.18 Esaïe 51.12
7 Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.
Ezéchiel 3.10 Jérémie 23.28 Ezéchiel 3.17 Jérémie 1.7 Jérémie 1.17
8 Bali wewe, mwanadamu, sikia neno hili ninalokuambia; usiwe wewe mwenye kuasi kama nyumba ile yenye kuasi; funua kinywa chako, ule nikupacho.
Apocalypse 10.9 Jérémie 15.16 Esaïe 50.5 1 Timothée 4.14-4.16 Lévitique 10.3
9 Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake.
Ezéchiel 8.3 Ezéchiel 3.1 Daniel 10.10 Apocalypse 10.8-10.11 Apocalypse 5.1-5.5
10 Akalikunjua mbele yangu; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; ndani yake yalikuwa yameandikwa maombolezo, na vilio, na ole!
Apocalypse 8.13 Esaïe 3.11 Apocalypse 9.12 Apocalypse 11.14 Jérémie 36.29-36.32