Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Deutéronome 34
Bible en Swahili de l’est


1 Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. Bwana akamwonyesha nchi yote ya Gileadi hata Dani; Deutéronome 32.49 Josué 19.47 Nombres 27.12 Juges 18.29 Genèse 14.14
2 na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi; Deutéronome 11.24 Josué 15.12 Nombres 34.6 Exode 23.31
3 na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari. Juges 3.13 Juges 1.16 2 Chroniques 28.15 Genèse 14.2 Genèse 19.22
4 Bwana akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko. Genèse 12.7 Genèse 28.13 Deutéronome 32.52 Genèse 26.3 Psaumes 105.9-105.11
5 Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana. Deutéronome 32.50 Josué 1.1-1.2 2 Pierre 1.1 Apocalypse 15.3 Jean 8.35-8.36
6 Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo. Jude 1.9 Deutéronome 3.29
7 Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka. Deutéronome 31.2 Genèse 27.1 Genèse 48.10 Josué 14.10-14.11 Actes 7.23
8 Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha. Genèse 50.3 Nombres 20.29 Genèse 50.10 Actes 8.2 Esaïe 57.1
9 Na Yoshua, mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama Bwana alivyomwamuru Musa. Esaïe 11.2 Daniel 6.3 Actes 6.6 Nombres 27.18-27.23 Jean 3.34
10 Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso; Exode 33.11 Deutéronome 18.15-18.18 Hébreux 3.5-3.6 Deutéronome 5.4-5.5 Actes 3.22-3.23
11 katika ishara zote na maajabu yote, ambayo Bwana alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote; Deutéronome 4.34 Deutéronome 7.19 Psaumes 105.26-105.38 Psaumes 78.43-78.58
12 na katika ule mkono wa nguvu wote, tena katika ule utisho mkuu wote, alioutenda Musa machoni pa Israeli wote.

Cette Bible est dans le domaine public.