Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

3 Jean 1.12
Bible en Swahili de l’est


1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.1 Jean 3.18 1 Corinthiens 1.14 Romains 16.23 Actes 20.4 2 Jean 1.1-1.13
2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.2 Pierre 1.3-1.9 Jacques 5.12 2 Pierre 3.18 3 Jean 1.3-1.6 Psaumes 20.1-20.5
3 Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.2 Jean 1.4 Ephésiens 1.15-1.16 2 Jean 1.2 3 Jean 1.4 Romains 1.8-1.9
4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.Philémon 1.10 Galates 4.19 2 Rois 20.3 1 Rois 3.6 2 Timothée 1.2
5 Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao,2 Corinthiens 4.1-4.3 Luc 12.42 1 Pierre 4.10-4.11 Luc 16.10-16.12 Galates 6.10
6 waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu.1 Thessaloniciens 2.12 Tite 3.13 Actes 15.3 Jonas 4.4 Colossiens 1.10
7 Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa.2 Rois 5.20-5.27 2 Corinthiens 12.13 2 Corinthiens 4.5 1 Corinthiens 9.18 Actes 8.4
8 Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.3 Jean 1.10 Philémon 1.24 Colossiens 4.11 1 Corinthiens 3.5-3.9 1 Thessaloniciens 3.2
9 Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.Luc 9.48 Matthieu 20.20-20.28 Luc 22.24-22.27 Tite 1.7-1.16 Matthieu 23.4-23.8
10 Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.Proverbes 10.10 3 Jean 1.5 2 Corinthiens 13.2 Esaïe 66.5 Luc 6.22
11 Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.Esaïe 1.16-1.17 Psaumes 37.27 1 Jean 2.29 2 Timothée 3.10 1 Pierre 3.13
12 Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Nasi pia twashuhudia, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.1 Timothée 3.7 Jean 21.24 Jean 19.35 Actes 10.22 1 Thessaloniciens 4.12
13 Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu.2 Jean 1.12
14 Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema uso kwa uso. [15] Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.Romains 16.1-16.16 Genèse 43.23 1 Pierre 5.14 Galates 5.16 Ephésiens 6.23

Cette Bible est dans le domaine public.