Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 14
Bible en Swahili de l’est


1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. Psaumes 10.4 Romains 3.10-3.12 Romains 1.21-1.32 Genèse 6.5 Luc 12.20
2 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. Psaumes 33.13-33.14 Genèse 6.12 Romains 3.11 Hébreux 11.6 2 Chroniques 19.3
3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja. Romains 3.10-3.12 Job 14.4 Esaïe 59.13-59.15 Esaïe 64.6 Esaïe 53.6
4 Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti Bwana. Esaïe 64.7 Jérémie 10.25 Psaumes 79.6 Amos 8.4 Psaumes 27.2
5 Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki. Psaumes 73.15 Psaumes 112.2 Psaumes 24.6 1 Pierre 2.9 Esaïe 41.10
6 Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge, Bali Bwana ndiye aliye kimbilio lake. Psaumes 9.9 Psaumes 42.10 Psaumes 4.2 Ezéchiel 35.10 Daniel 3.15
7 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! Bwana awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi. Psaumes 53.6 Psaumes 85.1

Cette Bible est dans le domaine public.