Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 146.2 Bible en Swahili de l’est
1 Haleluya. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.2 Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.3 Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake. 4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea. 5 Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake, 6 Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele, 7 Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; Bwana hufungua waliofungwa; 8 Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki; 9 Bwana huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huipotosha. 10 Bwana atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi. Haleluya.