Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 146.2
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.Psaumes 103.1 Psaumes 104.35 Psaumes 103.22-104.1 Psaumes 105.45
2 Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.Psaumes 104.33 Psaumes 63.4 Psaumes 71.14-71.15 Psaumes 145.1-145.2 Apocalypse 7.9-7.17
3 Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.Psaumes 118.8-118.9 Esaïe 2.22 Psaumes 108.12 Esaïe 37.6 Jérémie 17.5-17.6
4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.Psaumes 104.29 Ecclésiaste 12.7 Genèse 2.7 1 Corinthiens 2.6 Genèse 3.19
5 Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake,Psaumes 144.15 Jérémie 17.7-17.8 Psaumes 71.5 Psaumes 33.12 Exode 3.6
6 Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele,Apocalypse 14.7 Psaumes 100.5 Psaumes 117.2 Psaumes 89.2 Tite 1.2
7 Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; Bwana hufungua waliofungwa;Psaumes 103.6 Psaumes 68.6 Esaïe 61.1 Zacharie 9.11-9.12 Jérémie 31.14
8 Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki;Matthieu 9.30 Psaumes 145.14 Psaumes 11.7 Psaumes 147.6 Jean 14.21-14.23
9 Bwana huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huipotosha.Psaumes 68.5 Jérémie 49.11 Psaumes 147.6 2 Samuel 17.23 Esther 7.10
10 Bwana atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi. Haleluya.Psaumes 10.16 Exode 15.18 Joël 3.17 Daniel 2.44 Esaïe 52.7

Cette Bible est dans le domaine public.