Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 21.1
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana. 2 Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake. 3 Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. 4 Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. 5 Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake. 6 Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako. 7 Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa. 8 Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. 9 Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala. 10 Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi, Na wazao wao katika wanadamu. 11 Madhali walinuia kukutenda mabaya, Waliwaza hila wasipate kuitimiza. 12 Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale. 13 Ee Bwana, utukuzwe kwa nguvu zako, Nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako.

Cette Bible est dans le domaine public.