Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 32.9
Bible en Swahili de l’est


1 Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.Romains 4.6-4.8 Psaumes 85.2 Actes 13.38-13.39 Esaïe 44.22 Psaumes 40.4
2 Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.Jean 1.47 2 Corinthiens 1.12 1 Pierre 2.1-2.2 2 Corinthiens 5.19-5.21 Lévitique 17.4
3 Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa Kwa kuugua kwangu mchana kutwa.Psaumes 38.8 Psaumes 22.1 Psaumes 51.8 Lamentations 3.4 Luc 15.15-15.16
4 Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.Job 33.7 Psaumes 22.15 Psaumes 102.3-102.4 1 Samuel 5.11 Lamentations 5.10
5 Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.2 Samuel 12.13 Esaïe 65.24 Proverbes 28.13 Psaumes 38.18 Job 33.27
6 Kwa hiyo kila mtu mtauwa Akuombe wakati unapopatikana. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye.Esaïe 55.6 Esaïe 43.2 Psaumes 42.7 2 Corinthiens 6.2 Psaumes 34.2-34.5
7 Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, Utanizungusha nyimbo za wokovu.Psaumes 9.9 Psaumes 119.114 Psaumes 31.20 Juges 5.1 Psaumes 18.5
8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.Matthieu 11.29 Proverbes 3.5-3.6 Psaumes 33.18 Esaïe 49.10 Proverbes 8.10-8.11
9 Msiwe kama farasi wala nyumbu, Walio hawana akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.Proverbes 26.3 Jacques 4.7-4.10 Job 35.11 Jacques 3.3 Jérémie 8.6-8.7
10 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye Bwana fadhili zitamzunguka.Proverbes 16.20 Proverbes 13.21 Psaumes 34.8 Psaumes 16.4 Psaumes 5.12
11 Mfurahieni Bwana; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.Psaumes 64.10 Psaumes 68.3 Philippiens 4.4 Psaumes 97.12 Psaumes 33.1

Cette Bible est dans le domaine public.