1 Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.Psaumes 98.4 Esaïe 55.12 Psaumes 106.47 Psaumes 47.5 Psaumes 46.1
2 Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
Psaumes 68.35 Deutéronome 7.21 Malachie 1.14 Psaumes 66.3-66.5 Psaumes 95.3
3 Atawatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu.
Psaumes 18.47 Psaumes 81.14 1 Corinthiens 15.25 Psaumes 110.1 Josué 21.44
4 Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.
1 Pierre 1.4 Nahum 2.2 Amos 8.7 Amos 6.8 1 Jean 4.9-4.10
5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti ya baragumu.
Psaumes 68.33 2 Samuel 6.15 Psaumes 150.3 Psaumes 24.7-24.10 Luc 24.51-24.53
6 Mwimbieni Mungu, naam, imbeni; Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.
Matthieu 25.34 Matthieu 27.37 Esaïe 12.4-12.6 Psaumes 96.1-96.2 1 Chroniques 16.9
7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili.
Zacharie 14.9 Colossiens 3.16 1 Corinthiens 14.14-14.15 Apocalypse 11.15 Psaumes 47.2
8 Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.
1 Chroniques 16.31 Psaumes 9.4 Psaumes 89.14 Apocalypse 19.6 Psaumes 110.6
9 Wakuu wa watu wamekusanyika, Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana.
Psaumes 89.18 Romains 4.11-4.12 Psaumes 72.11 Matthieu 22.32 Esaïe 49.7