Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 47
Bible en Swahili de l’est


1 Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe. Psaumes 98.4 Esaïe 55.12 Psaumes 46.1 2 Rois 11.12 1 Samuel 10.24
2 Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. Deutéronome 7.21 Malachie 1.14 Psaumes 68.35 Psaumes 99.3 Psaumes 65.5
3 Atawatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu. Psaumes 18.47 1 Corinthiens 15.25 Psaumes 110.1 Psaumes 81.14 Deutéronome 33.29
4 Atatuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda. 1 Pierre 1.4 Nahum 2.2 Amos 6.8 Amos 8.7 Osée 14.4
5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti ya baragumu. Psaumes 68.33 Psaumes 24.7-24.10 2 Samuel 6.15 Psaumes 150.3 Psaumes 68.24-68.25
6 Mwimbieni Mungu, naam, imbeni; Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni. Matthieu 25.34 Psaumes 68.4 1 Chroniques 29.20 Psaumes 149.1-149.3 Exode 15.21
7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili. Zacharie 14.9 Colossiens 3.16 1 Corinthiens 14.14-14.15 Psaumes 47.8 Apocalypse 11.15
8 Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. 1 Chroniques 16.31 Psaumes 94.20 Hébreux 4.16 Psaumes 22.27-22.29 Psaumes 93.1
9 Wakuu wa watu wamekusanyika, Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana. Psaumes 89.18 Romains 4.11-4.12 Psaumes 72.11 Esaïe 60.4-60.5 Psaumes 72.7-72.9

Cette Bible est dans le domaine public.