Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 56.3
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza, Mchana kutwa ananionea akileta vita.Psaumes 69.13-69.16 Psaumes 57.1-57.3 Psaumes 16.1 Psaumes 27.2 Lamentations 2.16
2 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi.Psaumes 35.1 Actes 4.25-4.27 Psaumes 93.4 Psaumes 92.1 Psaumes 54.5
3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;Psaumes 55.4-55.5 Psaumes 34.4 1 Samuel 30.6 2 Corinthiens 7.5-7.6 Psaumes 11.1
4 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini?Psaumes 118.6 Hébreux 13.6 Psaumes 27.1 Psaumes 56.10-56.11 Psaumes 119.160
5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.2 Pierre 3.16 Psaumes 41.7 1 Samuel 18.29 Esaïe 29.20-29.21 1 Samuel 20.7
6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.Psaumes 71.10 Psaumes 59.3 Psaumes 140.2 Actes 4.5-4.6 Psaumes 37.32
7 Je! Wataokoka kwa uovu wao? Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.Psaumes 55.23 Jérémie 10.25 Esaïe 28.15 Jérémie 18.19-18.23 Psaumes 55.15
8 Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?)Psaumes 39.12 2 Rois 20.5 Malachie 3.16 Psaumes 139.16 Apocalypse 7.17
9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;Romains 8.31 Psaumes 118.6 Psaumes 102.2 Psaumes 46.11 Jérémie 33.3
10 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake.Hébreux 6.18 2 Pierre 1.4 Matthieu 24.35 Psaumes 60.6 Psaumes 56.4
11 Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?Psaumes 112.7-112.8 Esaïe 51.7-51.8 Esaïe 51.12-51.13 Psaumes 27.1
12 Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.Psaumes 9.1-9.3 Psaumes 50.14 Genèse 35.1-35.3 Genèse 28.20-28.22 1 Samuel 1.24-1.28
13 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.Job 33.30 Psaumes 116.8-116.9 Jean 8.12 Psaumes 17.5 Psaumes 145.14

Cette Bible est dans le domaine public.