Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 56
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza, Mchana kutwa ananionea akileta vita. Psaumes 69.13-69.16 Psaumes 57.1-57.3 Psaumes 16.1 Psaumes 27.2 Psaumes 35.25
2 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi. Psaumes 54.5 Psaumes 9.2 Psaumes 3.1 Psaumes 57.3 Psaumes 118.10-118.12
3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe; Psaumes 55.4-55.5 Psaumes 34.4 1 Samuel 30.6 1 Samuel 21.10 1 Samuel 21.12
4 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini? Psaumes 118.6 Hébreux 13.6 Psaumes 56.10-56.11 Psaumes 119.160 Psaumes 27.1
5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya. 2 Pierre 3.16 1 Samuel 20.7 Matthieu 22.15 Matthieu 26.61 1 Samuel 20.33
6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu. Psaumes 59.3 Psaumes 71.10 Psaumes 140.2 Luc 20.20 Job 14.16
7 Je! Wataokoka kwa uovu wao? Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako. Psaumes 55.23 Psaumes 55.15 Psaumes 94.20-94.21 Jérémie 7.10 Habakuk 1.13
8 Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?) Psaumes 39.12 2 Rois 20.5 Malachie 3.16 Matthieu 10.30 Psaumes 139.16
9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu; Romains 8.31 Psaumes 118.6 Psaumes 102.2 Jean 18.6 Psaumes 27.2
10 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake. Psaumes 56.4 Genèse 32.11 Hébreux 6.18 2 Pierre 1.4 Matthieu 24.35
11 Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? Esaïe 51.12-51.13 Psaumes 112.7-112.8 Esaïe 51.7-51.8 Psaumes 27.1
12 Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru. Psaumes 50.14 Psaumes 9.1-9.3 Esaïe 12.1 Psaumes 116.14-116.19 1 Samuel 1.11
13 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai. Psaumes 116.8-116.9 Job 33.30 Ephésiens 5.8-5.14 Esaïe 2.5 Jacques 5.20

Cette Bible est dans le domaine public.