Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 95.10 Bible en Swahili de l’est
1 Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. 2 Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. 3 Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote. 4 Mkononi mwake zimo bonde za dunia, Hata vilele vya milima ni vyake. 5 Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu. 6 Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba. 7 Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! 8 Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani. 9 Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.10 Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile, Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo, Hawakuzijua njia zangu.11 Nikaapa kwa hasira yangu Wasiingie rahani mwangu.