Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 15.2
Bible en Swahili de l’est


1 Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.Ezéchiel 25.8-25.11 Esaïe 11.14 Amos 2.1-2.3 Nombres 21.28 Esaïe 14.28
2 Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.Jérémie 48.1 Lévitique 21.5 Jérémie 48.18 Esaïe 3.24 Deutéronome 34.1
3 Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya dari zao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.Jonas 3.6-3.8 2 Rois 6.30 Esaïe 22.4 2 Samuel 3.31 Jérémie 19.13
4 Heshboni analia na Eleale; mpaka Yahasa sauti ya kulia kwao inasikiwa; hata watu wa Moabu waliovaa silaha wanapiga kelele sana kwa sababu hiyo; nafsi yake inatetemeka ndani yake.Jérémie 48.34 Nombres 21.23 Jérémie 20.18 Apocalypse 9.6 Josué 13.18
5 Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanapaliza sauti ya kukata tamaa.Jérémie 48.5 Jérémie 4.20 2 Samuel 15.23 Luc 19.41-19.44 Jérémie 13.17
6 Kwa maana maji ya Nimrimu yamekuwa mahali palipoharibika, kwa kuwa majani yamekauka, miche imenyauka, majani mabichi yamekoma.Nombres 32.36 Joël 1.10-1.12 Habakuk 3.17-3.18 Jérémie 48.34 Esaïe 19.5-19.7
7 Kwa hiyo vitu walivyojipatia tele, na akiba yao, wanavichukua hata kijito cha mierebi.Jérémie 48.36 Esaïe 10.6 Esaïe 30.6 Esaïe 10.14 Esaïe 5.29
8 Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.Esaïe 15.2-15.5 Jérémie 48.20-48.24 Ezéchiel 47.10 Jérémie 48.31-48.34
9 Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninaweka tayari msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao.2 Rois 17.25 Jérémie 50.17 Jérémie 15.3 Lévitique 26.18 Amos 5.19

Cette Bible est dans le domaine public.