Prophétie sur Moab
1 Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.
Esaïe 11.14 Amos 2.1-2.3 Nombres 21.28 Ezéchiel 25.8-25.11 Esaïe 14.28
2 Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.
Jérémie 48.1 Lévitique 21.5 Jérémie 48.18 Esaïe 3.24 Deutéronome 34.1
3 Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya dari zao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.
Jonas 3.6-3.8 2 Samuel 3.31 Jérémie 19.13 Matthieu 11.21 Deutéronome 22.8
4 Heshboni analia na Eleale; mpaka Yahasa sauti ya kulia kwao inasikiwa; hata watu wa Moabu waliovaa silaha wanapiga kelele sana kwa sababu hiyo; nafsi yake inatetemeka ndani yake.
Jérémie 48.34 Jérémie 20.18 Apocalypse 9.6 Josué 13.18 Nombres 11.15
5 Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanapaliza sauti ya kukata tamaa.Jérémie 48.5 Jérémie 4.20 Jérémie 13.17 Jérémie 9.10 Esaïe 22.5
6 Kwa maana maji ya Nimrimu yamekuwa mahali palipoharibika, kwa kuwa majani yamekauka, miche imenyauka, majani mabichi yamekoma.
Joël 1.10-1.12 Nombres 32.36 Jérémie 48.34 Esaïe 19.5-19.7 Josué 13.27
7 Kwa hiyo vitu walivyojipatia tele, na akiba yao, wanavichukua hata kijito cha mierebi.
Jérémie 48.36 Esaïe 10.14 Esaïe 5.29 Psaumes 137.1-137.2 Nahum 2.12-2.13
8 Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.
Jérémie 48.20-48.24 Ezéchiel 47.10 Jérémie 48.31-48.34 Esaïe 15.2-15.5
9 Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninaweka tayari msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao.
2 Rois 17.25 Lévitique 26.18 Amos 5.19 Jérémie 48.43-48.45 Lévitique 26.24