1 Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini. Esaïe 51.9 Esaïe 66.16 Psaumes 104.26 Job 26.13 Apocalypse 12.3-13.2 Annonce du rétablissement d’Israël 2 Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.
Jérémie 2.21 Luc 20.9-20.18 Psaumes 80.8-80.19 Esaïe 5.1-5.7 Nombres 21.17 3 Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.
Esaïe 58.11 1 Samuel 2.9 Psaumes 46.5 Ezéchiel 37.28 Psaumes 46.11 4 Hasira sinayo ndani yangu; Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.
Esaïe 10.17 Hébreux 6.8 Matthieu 3.12 2 Samuel 23.6 Esaïe 12.1 5 Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami.
Esaïe 25.4 Job 22.21 Esaïe 57.19 Ezéchiel 34.25-34.26 Luc 14.32 6 Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
Esaïe 37.31 Osée 14.5-14.6 Romains 11.16-11.26 Jérémie 30.19 Apocalypse 11.15 7 Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?
Esaïe 37.36-37.38 Daniel 2.31-2.35 Esaïe 17.3 Jérémie 50.40 Nahum 1.14 8 Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.
Jérémie 10.24 Osée 13.15 Ezéchiel 19.12 Jérémie 4.11 Jérémie 4.27 9 Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
Romains 11.27 Esaïe 48.10 Daniel 11.35 Esaïe 17.8 2 Chroniques 36.19 10 Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake.
Esaïe 17.2 Jérémie 26.6 Michée 3.12 Esaïe 17.9 Esaïe 32.13-32.14 11 Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Esaïe 43.1 Jérémie 8.7 Esaïe 43.7 Esaïe 44.24 Esaïe 1.3 12 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
Genèse 15.18 Deutéronome 30.3-30.4 Néhémie 1.9 Esaïe 56.8 Psaumes 72.8 13 Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.
Matthieu 24.31 Lévitique 25.9 Esaïe 11.16 Hébreux 12.22 Zacharie 14.16