Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 27
Bible en Swahili de l’est


1 Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini. Esaïe 51.9 Esaïe 66.16 Psaumes 104.26 Job 26.13 Apocalypse 12.3-13.2
2 Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni. Jérémie 2.21 Luc 20.9-20.18 Psaumes 80.8-80.19 Esaïe 5.1-5.7 Nombres 21.17
3 Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda. Esaïe 58.11 1 Samuel 2.9 Psaumes 46.5 Ezéchiel 37.28 Psaumes 46.11
4 Hasira sinayo ndani yangu; Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja. Esaïe 10.17 Hébreux 6.8 Matthieu 3.12 2 Samuel 23.6 Esaïe 12.1
5 Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami. Esaïe 25.4 Job 22.21 Esaïe 57.19 Ezéchiel 34.25-34.26 Luc 14.32
6 Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda. Esaïe 37.31 Osée 14.5-14.6 Romains 11.16-11.26 Jérémie 30.19 Apocalypse 11.15
7 Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye? Esaïe 37.36-37.38 Daniel 2.31-2.35 Esaïe 17.3 Jérémie 50.40 Nahum 1.14
8 Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki. Jérémie 10.24 Osée 13.15 Ezéchiel 19.12 Jérémie 4.11 Jérémie 4.27
9 Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena. Romains 11.27 Esaïe 48.10 Daniel 11.35 Esaïe 17.8 2 Chroniques 36.19
10 Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake. Esaïe 17.2 Jérémie 26.6 Michée 3.12 Esaïe 17.9 Esaïe 32.13-32.14
11 Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe. Esaïe 43.1 Jérémie 8.7 Esaïe 43.7 Esaïe 44.24 Esaïe 1.3
12 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli. Genèse 15.18 Deutéronome 30.3-30.4 Néhémie 1.9 Esaïe 56.8 Psaumes 72.8
13 Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu. Matthieu 24.31 Lévitique 25.9 Esaïe 11.16 Hébreux 12.22 Zacharie 14.16

Cette Bible est dans le domaine public.