Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 27.8
Bible en Swahili de l’est


1 Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.Esaïe 66.16 Esaïe 51.9 Psaumes 104.26 Job 26.13 Apocalypse 12.3-13.2
2 Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.Jérémie 2.21 Luc 20.9-20.18 Psaumes 80.8-80.19 Esaïe 5.1-5.7 Nombres 21.17
3 Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.Esaïe 58.11 1 Samuel 2.9 Esaïe 60.16 Ezéchiel 37.14 Esaïe 41.13-41.19
4 Hasira sinayo ndani yangu; Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.Esaïe 10.17 Hébreux 6.8 Matthieu 3.12 2 Samuel 23.6 Psaumes 103.9
5 Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami.Esaïe 25.4 Job 22.21 2 Corinthiens 5.19-5.21 Osée 2.18-2.20 Esaïe 26.3-26.4
6 Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.Osée 14.5-14.6 Esaïe 37.31 Zacharie 10.8-10.9 Esaïe 6.13 Zacharie 2.11
7 Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?Esaïe 37.36-37.38 Nahum 1.14 Jérémie 50.33-50.34 Esaïe 17.14 Esaïe 10.20-10.25
8 Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.Jérémie 10.24 Osée 13.15 Ezéchiel 19.12 Jérémie 4.11 Psaumes 103.14
9 Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.Esaïe 48.10 Daniel 11.35 Esaïe 17.8 Romains 11.27 Ezéchiel 24.11-24.14
10 Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake.Esaïe 17.2 Michée 3.12 Esaïe 17.9 Esaïe 32.13-32.14 Jérémie 26.18
11 Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.Esaïe 43.1 Jérémie 8.7 Esaïe 43.7 Esaïe 44.24 Esaïe 1.3
12 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.Genèse 15.18 Néhémie 1.9 Esaïe 56.8 Deutéronome 30.3-30.4 Amos 9.9
13 Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.Matthieu 24.31 Lévitique 25.9 Esaïe 11.16 Hébreux 12.22 Zacharie 14.16

Cette Bible est dans le domaine public.