1 Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Esaïe 66.16 Esaïe 51.9 Psaumes 104.26 Job 26.13 Apocalypse 12.3-13.2 Annonce du rétablissement d’Israël 2 Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.
Jérémie 2.21 Luc 20.9-20.18 Psaumes 80.8-80.19 Esaïe 5.1-5.7 Nombres 21.17 3 Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.
Esaïe 58.11 1 Samuel 2.9 Esaïe 41.13-41.19 Psaumes 121.3-121.5 Esaïe 46.4 4 Hasira sinayo ndani yangu; Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.
Esaïe 10.17 Hébreux 6.8 Matthieu 3.12 2 Samuel 23.6 Esaïe 54.6-54.10 5 Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami.
Esaïe 25.4 Job 22.21 Esaïe 26.3-26.4 Luc 19.42 Luc 13.34 6 Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
Osée 14.5-14.6 Esaïe 37.31 Zacharie 2.11 Esaïe 49.20-49.23 Osée 2.23 7 Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?
Esaïe 37.36-37.38 Nahum 1.14 Jérémie 50.33-50.34 Esaïe 17.14 Esaïe 10.20-10.25 8 Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki. Osée 13.15 Ezéchiel 19.12 Jérémie 4.11 Jérémie 10.24 Esaïe 10.12 9 Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
Esaïe 48.10 Daniel 11.35 Esaïe 17.8 Romains 11.27 Hébreux 12.6 10 Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake.
Esaïe 17.2 Michée 3.12 Esaïe 17.9 Esaïe 32.13-32.14 Jérémie 26.18 11 Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Jérémie 8.7 Esaïe 43.7 Esaïe 44.24 Esaïe 1.3 Esaïe 43.1 12 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
Genèse 15.18 Néhémie 1.9 Esaïe 56.8 Deutéronome 30.3-30.4 Luc 15.4 13 Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.
Matthieu 24.31 Lévitique 25.9 Zacharie 14.16 Esaïe 19.23-19.25 1 Chroniques 15.24