1 Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.
Matthieu 3.2 Psaumes 85.9 Esaïe 46.13 Psaumes 24.4-24.6 Romains 1.17
2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote.
Esaïe 58.13 Exode 31.13-31.16 Ezéchiel 20.20 Jérémie 17.21-17.22 Ezéchiel 20.12
3 Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu.
Romains 15.16 Jérémie 50.5 Esaïe 14.1 Jérémie 39.16-39.17 Ephésiens 2.12
4 Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu;
Esaïe 56.6 Jérémie 50.5 Psaumes 119.111 Esaïe 27.5 Luc 10.42
5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali.
Esaïe 55.13 Jean 1.12 1 Timothée 3.15 Apocalypse 3.12 Matthieu 16.18
6 Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;
Apocalypse 1.10 Jacques 2.5 Ephésiens 6.24 Esaïe 60.10 Marc 12.30-12.34
7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.Marc 11.17 Luc 19.46 Matthieu 21.13 Malachie 1.11 Esaïe 2.2-2.3
8 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Jean 10.16 Esaïe 60.3-60.11 Jérémie 31.10 Esaïe 66.18-66.21 Zacharie 10.8-10.10
9 Enyi hayawani wote wa nyikani, njoni, Mle, enyi hayawani wote wa mwituni.
Jérémie 12.9 Apocalypse 19.17-19.18 Esaïe 18.6 Ezéchiel 29.5 Deutéronome 28.26
10 Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.
Philippiens 3.2 Esaïe 29.10 Jérémie 14.13-14.14 Nahum 3.18 Proverbes 6.4-6.10
11 Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.
Ezéchiel 13.19 Michée 3.11 Michée 3.5-3.6 Esaïe 1.3 Tite 1.7
12 Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi.
Esaïe 5.22 Psaumes 10.6 1 Corinthiens 15.32 Luc 12.19-12.20 Proverbes 23.35