Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 8
Bible en Swahili de l’est


1 Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya Bwana; kwa sababu wamelihalifu agano langu, wameiasi sheria yangu. Osée 6.7 Deutéronome 28.49 Osée 5.8 Jérémie 4.13 Habakuk 1.8
2 Watanililia, Mungu wangu, sisi Israeli tunakujua. Matthieu 7.21 Tite 1.16 1 Jean 2.4 Luc 13.25 Psaumes 78.34-78.37
3 Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia. Deutéronome 28.25 Lamentations 3.66 Lévitique 26.36 Amos 1.11 Psaumes 36.3
4 Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali. Osée 2.8 Osée 13.2 2 Rois 15.10-15.30 Jean 10.14 Ezéchiel 18.31
5 Amemtupa ndama yako, Ee Samaria; hasira yangu imewaka juu yao; siku ngapi zitapita kabla ya hao kupata hali isiyo na hatia? Osée 10.5 Jérémie 13.27 Deutéronome 32.22 Osée 8.6 Jérémie 4.14
6 Maana katika Israeli kimetokea hata na kitu hiki; fundi ndiye aliyekifanya, nacho si mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria itavunjika vipande vipande. 2 Chroniques 34.6-34.7 Actes 17.29 Habakuk 2.18 Jérémie 50.2 Jérémie 43.12-43.13
7 Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza. Proverbes 22.8 Job 4.8 Galates 6.7 Osée 7.9 Jérémie 12.13
8 Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza. Jérémie 22.28 Jérémie 51.34 Jérémie 48.38 Lamentations 2.16 2 Timothée 2.20-2.21
9 Kwa maana wamekwea kwenda Ashuru, mfano wa punda wa mwituni aliye peke yake; Efraimu ameajiri wapenzi. Jérémie 2.24 Osée 7.11 Osée 5.13 Ezéchiel 16.33-16.34 Esaïe 30.6
10 Naam, ijapokuwa waajiri kati ya mataifa, sasa nitawakusanya; nao wanaanza kupunguka kwa sababu ya mzigo wa mfalme wa wakuu. Ezéchiel 16.37 Ezéchiel 26.7 Esaïe 10.8 Osée 10.10 Ezéchiel 22.20
11 Kwa kuwa Efraimu ameongeza madhabahu kwa dhambi, madhabahu zimekuwa dhambi kwake. Osée 12.11 Osée 10.8 Jérémie 16.13 Esaïe 10.10-10.11 Osée 10.1-10.2
12 Nijapomwandikia sheria yangu katika amri elfu kumi, zimehesabiwa kuwa ni kitu kigeni. Osée 4.6 Esaïe 30.9 Psaumes 119.18 Néhémie 9.13-9.14 Psaumes 50.17
13 Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini Bwana hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri. Osée 9.6 Osée 9.9 Deutéronome 28.68 Amos 5.22 Jérémie 14.10
14 Maana Israeli amemsahau Muumba wake, naye amejenga nyumba za enzi; na Yuda ameongeza miji yenye maboma; lakini nitapeleka moto juu ya miji yake, nao utaziteketeza ngome zake. Deutéronome 32.18 Jérémie 17.27 Amos 2.5 Osée 13.6 2 Chroniques 27.4

Cette Bible est dans le domaine public.