Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 8.9
Bible en Swahili de l’est


1 Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya Bwana; kwa sababu wamelihalifu agano langu, wameiasi sheria yangu.Osée 6.7 Deutéronome 28.49 Osée 5.8 Jérémie 4.13 Habakuk 1.8
2 Watanililia, Mungu wangu, sisi Israeli tunakujua.Tite 1.16 Matthieu 7.21 Esaïe 48.1-48.2 Jérémie 7.4 Osée 7.13-7.14
3 Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia.Deutéronome 28.25 Lamentations 3.66 Lévitique 26.36 Amos 1.11 Psaumes 36.3
4 Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.Osée 13.2 Osée 2.8 2 Rois 15.10-15.30 Osée 13.9-13.10 Luc 13.27
5 Amemtupa ndama yako, Ee Samaria; hasira yangu imewaka juu yao; siku ngapi zitapita kabla ya hao kupata hali isiyo na hatia?Osée 10.5 Jérémie 13.27 Deutéronome 32.22 Osée 8.6 Jérémie 4.14
6 Maana katika Israeli kimetokea hata na kitu hiki; fundi ndiye aliyekifanya, nacho si mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria itavunjika vipande vipande.Actes 19.26 2 Chroniques 31.1 Osée 10.2 Jérémie 10.3-10.9 2 Chroniques 34.6-34.7
7 Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.Proverbes 22.8 Job 4.8 Galates 6.7 Osée 7.9 Juges 6.3-6.6
8 Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza.Jérémie 22.28 Jérémie 51.34 2 Rois 17.1-17.6 Deutéronome 28.64 Esaïe 30.14
9 Kwa maana wamekwea kwenda Ashuru, mfano wa punda wa mwituni aliye peke yake; Efraimu ameajiri wapenzi.Jérémie 2.24 Osée 7.11 Osée 5.13 Ezéchiel 16.33-16.34 2 Rois 15.19
10 Naam, ijapokuwa waajiri kati ya mataifa, sasa nitawakusanya; nao wanaanza kupunguka kwa sababu ya mzigo wa mfalme wa wakuu.Ezéchiel 16.37 Ezéchiel 26.7 Esaïe 10.8 Ezéchiel 23.9-23.10 2 Rois 17.3
11 Kwa kuwa Efraimu ameongeza madhabahu kwa dhambi, madhabahu zimekuwa dhambi kwake.Osée 12.11 Osée 10.8 Jérémie 16.13 Esaïe 10.10-10.11 Osée 10.1-10.2
12 Nijapomwandikia sheria yangu katika amri elfu kumi, zimehesabiwa kuwa ni kitu kigeni.Osée 4.6 Néhémie 9.26 Psaumes 147.19-147.20 Proverbes 22.20 Jérémie 6.16-6.17
13 Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini Bwana hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.Osée 9.6 Osée 9.9 Deutéronome 28.68 Esaïe 1.11 Amos 5.22
14 Maana Israeli amemsahau Muumba wake, naye amejenga nyumba za enzi; na Yuda ameongeza miji yenye maboma; lakini nitapeleka moto juu ya miji yake, nao utaziteketeza ngome zake.Deutéronome 32.18 Jérémie 17.27 Amos 2.5 Osée 13.6 Psaumes 106.21

Cette Bible est dans le domaine public.