Prédication de Jonas à Ninive
1 Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema,
Jonas 1.1 Jean 21.15-21.17
2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru.
Ezéchiel 2.7 Jérémie 1.17 Jonas 1.2 Matthieu 3.8 Jérémie 15.19-15.21
3 Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu.
4 Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.
Deutéronome 18.22 Jérémie 18.7-18.10 2 Rois 20.1 2 Rois 20.6 Jonas 3.10
5 Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.
Luc 11.32 Matthieu 12.41 2 Chroniques 20.3 Daniel 9.3 Joël 1.14
6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
Esther 4.1-4.4 Job 2.8 Jacques 4.6-4.10 Ezéchiel 27.30-27.31 Luc 10.13
7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;
2 Chroniques 20.3 Joël 2.15-2.16 Esdras 8.21 Joël 1.18 Jonas 3.5
8 bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake.Esaïe 55.6-55.7 Jonas 1.6 Esaïe 1.16-1.19 Esaïe 59.6 Jonas 1.14
9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?
2 Samuel 12.22 Psaumes 106.45 Amos 5.15 Jonas 1.6 Joël 2.13-2.14
10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
Jérémie 18.8 Amos 7.6 Exode 32.14 Amos 7.3 1 Rois 21.27-21.29