Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Samuel 28.11
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa siku zile hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao waende vitani, ili kupigana na Israeli. Naye Akishi akamwambia Daudi, Jua hakika ya kuwa wewe utatoka pamoja nami jeshini, wewe na watu wako.1 Samuel 29.1-29.3 1 Samuel 17.1 1 Samuel 13.5 1 Samuel 27.12 Juges 3.1-3.4
2 Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinda kichwa changu daima.1 Samuel 27.10 2 Samuel 16.16-16.19 Romains 12.9
3 Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Israeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi.1 Samuel 25.1 Lévitique 20.27 Lévitique 19.31 Exode 22.18 Deutéronome 18.10-18.11
4 Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa.Josué 19.18 1 Samuel 31.1 2 Rois 4.8 2 Samuel 1.6 2 Samuel 21.12
5 Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana.Psaumes 48.5-48.6 Job 18.11 Psaumes 73.19 Esaïe 21.3-21.4 Daniel 5.6
6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.1 Samuel 14.37 Nombres 12.6 Nombres 27.21 Lamentations 2.9 Exode 28.30
7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.Josué 17.11 Actes 16.16 Psaumes 83.10 1 Chroniques 10.13 Lamentations 3.25-3.26
8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako.Esaïe 8.19 1 Chroniques 10.13 2 Chroniques 35.22 1 Rois 22.30 Deutéronome 18.10-18.11
9 Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua?1 Samuel 28.3 2 Samuel 18.13 2 Rois 5.7
10 Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili.1 Samuel 19.6 Genèse 3.5 Exode 20.7 1 Samuel 14.39 Matthieu 26.72
11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli. 12 Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli.1 Rois 14.5 1 Samuel 28.3
13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.Exode 4.16 Exode 22.28 Jean 10.34-10.35 Psaumes 82.6-82.7
14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.1 Samuel 15.27 2 Rois 2.8 2 Rois 2.13-2.14 1 Samuel 24.8
15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.1 Samuel 28.6 1 Samuel 18.12 Luc 16.23-16.26 1 Samuel 16.13-16.14 1 Samuel 28.11
16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?Apocalypse 18.20 Juges 5.31 Lamentations 2.5 Psaumes 68.1-68.3 2 Rois 6.27
17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.1 Samuel 15.27-15.29 1 Samuel 16.13 Proverbes 16.4 1 Samuel 24.20 1 Samuel 13.13-13.14
18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo.1 Rois 20.42 1 Samuel 15.9 1 Samuel 15.20 1 Chroniques 10.13 Jérémie 48.10
19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.Jérémie 28.16-28.17 1 Rois 22.20 Actes 5.9-5.10 Exode 9.18 Actes 5.5
20 Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha.1 Samuel 25.37 Job 26.2 Psaumes 50.21-50.22 Job 15.20-15.24 1 Samuel 28.5
21 Ndipo yule mwanamke akamwendea Sauli, akamwona ya kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako, nami nimeutia uhai wangu mkononi mwangu, nami nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia.Juges 12.3 Job 13.14 1 Samuel 19.5
22 Basi sasa, tafadhali, wewe uisikilize sauti ya mjakazi wako, nikakuandalie ngaa mkate kidogo; ukale, ili upate nguvu, utakapokwenda zako. 23 Lakini yeye alikataa, akasema, Mimi sitaki kula. Ila watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha; naye akaisikiliza sauti yao. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda.1 Rois 21.4 Luc 14.23 Actes 16.15 2 Rois 5.13 Luc 24.29
24 Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya mkate wa mofa kwa unga huo;Luc 15.23 Genèse 18.7-18.8
25 kisha akamwandalia Sauli na watumishi wake; wakala. Ndipo wakaondoka, wakaenda zao usiku ule.

Cette Bible est dans le domaine public.